Wednesday, 9 May 2012

MCHEZAJI WA IRELAND AFUNGA AKAUNTI YAKE YA TWITTER


Mcheza kandanda mashuhuri wa Ireland, James McClean ameripotiwa kufunga akaunti yake ya Twitter baada ya kupokea vitisho vya kifo kutoka kwa mashabiki. Mchezaji huyo ambaye pia ni winga wa timu ya Sunderland inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza(EPL),anadaiwa kuwakasirisha mashabiki wa Ireland kaskazini ambapo ndiyo asili yake  baada ya kuchagua kuichezea Jamuhuri ya Ireland katika mashindano ya Kombe la Ulaya(Euro 2012).Nyota huyo aliiwakilisha vema Ireland kaskazini katika mashindano ya vijana.