Wednesday, 28 September 2011

WANAMUZIKI WA TANZANIA WAIGE HII HAPA KWA MSECHU

Peter Msechu alipopata ushindi kwenye mashindano ya Tusker Project Fame Allstars watanzania wengi walifurahi. Wengi wao walifurahi ushindi na mambo mazuri aliyoyafanya akiwa katika safari yote ya kuelekea fainali ya mashindano hayo. Hiyo ni kwa mashabiki. Kwa wanamuziki wengine wa kitanzania wanatakiwa kuiga namna Msechu anvyojitahidi kufanya muziki ambao sio wa kusahulika kirahisi.Kwa kufanya hivyo tutafika mbali.