Thursday, 10 May 2012
DIAMOND KUFANYA SHOW KWENYE MSAKO WA MISS & MR IFM
Shindano la kuwatafuta Mr & Miss IFM linatarajiwa kufanyika jumamosi ya tarehe 12 mwezi huu katika ukumbi wa Cine Club Mikocheni. Shindano hilo la kumtafuta mlimbwede na mkaka mtanashati kutoka chuo hicho cha usimamizi wa fedha kitaambatana na show kali kutoka kwa msanii mkali wa bongo fleva ambaye nyota yake kwa sasa inangaa vibaya mno, Diamond Platnumz.Msanii huyo ambaye anamiliki tuzo sita za Kili mpaka sasa anategemewa kuifanya shughuli hiyo kuwa ya kusisimua kutokana na kujinyakulia idadi kubwa ya mashabiki siku za karibuni na aina yake ya muziki anyoileta kwa hadhira.Na pia mpenzi wake wa sasa Jokate Mwengelo hatakua nyuma kwani KIDOTI nao ni moja kati ya watu watakaofanikisha msako huo wa Mr & Miss IFM kukamilika.